Posts

Showing posts from September, 2021

RAIS SAMIA AMWAGA MABILIONI UJENZI WA OFISI ZA SANAA NA MICHEZO

Image
  Katibu Mkuu wa Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akionesha picha ya jenhgo jipya la Wizara hiyo mara baada ya kusaini Mkataba wa ujenzi wa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Septemba 22,2021 jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Sanaa, utamaduni na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi(kulia) wakikabidhiana Mikataba ya Ujenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani. Picha ya pamoja baina ya Katibu Mkuu na Menejimenti ya Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo katika pamoja na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) …………………………………………………………………………… Na John Mapepele- WSUM, Dodoma  Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kujengewa jengo la TZS Bilioni 22.843 makao makuu jijini Dodoma na mkataba wa ujenzi tayari umesainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Dkt. Maulid Banyani. Akizungumza katika hafla hiyo y...

RUBI, NANDY JUKWAA MOJA LEO TANZANITE FESTIVAL DAR

Image
  Msanii Ruby Msanii Nandy Na John Mapepele,Dar Wasanii mahiri wa kike ambao pia wamekuwa katika ushindani kimuziki Rubi na Nandy leo wataonesha kuwa wanawake wakiwa na lao wanaungana. Baada ya miaka mingi ya kukwepana na kila mmoja kuonekana anapania kufanya vizuri zaidi ya mwenzake leo Jumamosi, Septemba 18, 2021, Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite linawakutanisha kwenye Uwanja wa Uhuru hapa Dar es Salaam. Michezo mingi leo ikiwa ni siku ya tatu tayari imeanza asubuhi na itaendelea hadi jioni ambapo saa kumi jioni Simba Queen itaoneshana ubabe na Timu ya Taifa ya Wanawake U23 kwenye Uwanja huo wa Uhuru. “Wasanii zaidi ya 10 watakaopanda stejini leo wakiwemo Nandy na Rubi watu wajazane uwanjani kabla ya saa nane kwani baada ya hapo kutakuwa na ufunguzi na wasanii hawa watatumbuiza mpaka jioni,” ametangaza MC wa sherehe hizo jana jioni wakati wa mapambano ya ndodi uwanjani hapo.  Wasanii wengine wakali wa kike wanaotarajiwa kuwepo leo (wakisindikizwa na kaka yao mkali...

ZANZIBAR YANG’ARA MBIO FUPI KWENYE TAMASHA LA MICHEZO YA WANAWAKE LA TANZANITE

Image
  Na John Mapepele, Dsm   Zanzibar imeibuka mbabe katika mashindano ya mbio fupi uwanja wa Benjamini Mkapa kwenye maadhimisho yanayoendelea ya Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite leo Septemba 17, 2021ikiwa ni siku ya pili kabla ya kuzinduliwa rasmi kesho na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan   Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa uratibu wa mbio hizo, Robert Kalyahe amesema Zanzibar imeweza kuwa bingwa kwa mbio za mita mia moja katika nafasi zote tatu ambapo amesema mshindi wa kwanza kwenye mbio hizo ni Hynes Jolini aliyetumia sekunde 11:62 akifuatiwa na Winfrida Makenji aliyetumia sekunde 11:74 na nafasi ya tatu imekwenda kwa Kazija Hassan aliyetumia sekunde12:45.   Pia Kalyahe amesema katika mbio za mita mia mbili nafasi zote tatu zimenyakuliwa na washindi kutoka Zanzibar ambapo amesema Emma Hossea amenyakua nafasi ya kwanza kwa kutumia sekunde 24:82 na nafasi ya pili imechukuliwa na Nasra Abdallah aliyetumia sekunde 25:55 wakati nafasi ya tatu imekwenda kwa Neema Ally a...

PROF.MKUMBO AELEZA MSIMAMO WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA WTO

Image
  **************************************   TANZANIA imetaka kuwepo na uhuru wa kisera kwa nchi zinazoendelea na maskini ili kujihami na athari za uingizwaji uliokithiri wa bidhaa za kilimo hususan kutoka nchi zilizoendelea.   Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof.Kitila Mkumbo amesema hayo Septemba 16, 2021, katika Mkutano wa Mawaziri wa Kundi la Nchi 33 (G33) wa wanachama wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) uliofanyika kwa njia ya mtandao ambapo aliongoza ujumbe kutoka Tanzania.   Kundi hilo linajumuisha nchi wanachama zenye maslahi yanayofanana ya kutaka uwazi na manufaa katika majadiliano ya WTO yanayohusu Kilimo ambapo lengo la mkutano ni kujadili na kuweka msimamo wa pamoja katika maeneo ya kipaumbele kwenye kilimo.   Katika mchango wake, Mhe. Prof. Mkumbo amebainisha msimamo wa Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ambao unaungwa mkono na nchi nyingine wanachama kwenye eneo la misaada ya upendeleo (Domestic Support).   “Msimamo wa Tanzania ni kuwa na ...

CHONGOLO AANZA ZIARA MKOANI MTWARA LEO

Image
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wameanza ziara mkoani Mtwara yenye lengo la kukagua na kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 – 2025. Naibu Katibu Mkuu CCM bara Ndugu Christine Mdeme akipoungia. Mkono wananchi wakati wajumbe hao wa Sekretarieti ya CCM taifa walipowasili mkoani Mtwara leo. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka akiwasalimia wananchi wakati wajumbe wa Sekretarieti ya CCM taifa walipowasili mkoani Mtwara. Naibu Katibu Mkuu CCM bara Ndugu Christine Mdeme akiwasalimia wananchi wakati wajumbe hao wa Sekretarieti ya CCM taifa walipowasili mkoani Mtwara leo.

DKT. ABBASI AANIKA MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MICHEZO

Image
    Na. John Mapepele, Dsm Katibu Mkuu anayesimamia Sekta za Sanaa, Utamaduni na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa mchango mkubwa kwenye tasnia ya michezo hususan michezo ya wanawake katika hiki kifupi ikiwa madarakani kwa kuipa kipaombele michezo hiyo.  Dkt. Abbasi ameyasema hayo leo Septemba 16, 2021 katika siku ya kwanza kati ya siku tatu za Tamasha la Michezo ya Wanawake la Tanzanite lililoratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambapo amesema lengo la tamasha hili ni kutoa hamasa kwa wanamichezo wanawake kushiriki na kufanya vizuri kwenye michezo. Akifafanua baadhi ya michango mikubwa iliyotolewa na Serikali katika kipindi hiki kwenye tasnia ya michezo amesema ni pamoja na kutoa kiasi cha shilingi Bilioni 9.5 kwa ajili ya kujenga  viwanja vya  wazi vya michezo na kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kuzisaidia timu zote za taifa ikiwa ni pamoja na za wanawake. Amesema Serikali inakusudia kujenga ukum...